kabla hatujaendelea wenda kuna ndugu zetu wengine hawajui hata Adsense yenyewe ni nini soma hapa [ Jinsi ya kupata pesa kupitia Adsense ]
haya sasa tuendelee na mada yetu hii kwanza kabisa fahamu jinsi ya kuweka namna ya kupokea mapato yako kupitia Western Union ingia katika akaunti yako ya adsense
upande wa kushoto wa dashibodi ya adsense bonyeza sehemu iliyoandika setting kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Payment
kisha utabonyeza sehemu imeandikwa manager payment kisha ongeza au chagua western union kisha ifanye kuwa ndio Primary sasa rudi katika payment
Kama utaona muonekano kama huo pichani basi umefaulu sasa tuangalie vipi utaweza kuzishika pesa zako mikononi baada ya kufikia U$D 100 ambacho ndio kiwango cha adsense kuwalipa watumiaji wake.
Bonyeza hiyo sehemu iliyoandikwa View Transactions kisha tazama muamala wako kisha ubonyeze itafunguka new Tab itakuonesha kila kitu
hapo ndio ilipokuwa pesa yako hizo ndio vitu vya kuandika sehemu au kama utaenda na kifaa chako katika bank/ofisi inayotoa huduma za western union
RELATED ARTICLE
vitu vya kuzingatia wakati unaenda katika ofisi za western union kuchukua pesa yako ni lazima uende na na moja kati ya hivi: Passport ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha kitaifa au cha mpiga kura na lazima kiwe chako wewe mwenyewe.ukifika kuna karatasi utatakiwa kujaza majina yako ya utakayoyajaza lazima yafanane na ya katika kitambulisho chako na akaunti yako ya adsense, sehemu ya swali jaza namba zilizopo katika ID Billing tazama hapo pichani utaziona katika sehemu ya mtu anayekutumia jaza Google Ireland Limited.
Ukishafika kwa mtoa huduma mpe hiyo karatasi na kitambulisho chako kati ya ivo nilivyokuorodheshea hapo kwenye maandishi mekundu.
mpaka hapo utakuwa umekamilisha kuchukua pesa yako sasa furahiya, bila shaka umepata mwangaza kidogo kama sio sana lakini kama kuna sehemu hujaelewa niachie swali lako katika sehemu ya maoni nami nitakujibu kwa kadri nitakavyokuelewa. shukrani kwa kuwa nami mwanzo mpaka mwisho sambaza makala hii kwa ndugu na jamaa ili nao wafaidike
0 Comments