JINSI YA KUPOKEA PESA YAKO KUTOKA ADSENSE

Habari na karibu katika ukumbi huu maridhawa kwaajili yako , kutokana na maombi ya baadhi ya wasomaji wangu kuhitaji kufahamu jinsi ya kupokea pesa zao kutoka adsense leo nimeonelea wacha tujuzane kuhusu hili, ispokuwa nitaeleza kwa upande wa bank tu hizi njia nyingine tutaelezana wakati mwingine au hata kwa kupitia maoni.

kwanza fahamu jambo muhimu kuwa adsense wanawatumia pesa zao wateja wake kuanzia dola 100, pia ili kujua jinsi ya kurekebisha mambo mpaka pesa yako itumwe kwenye bank akaunti yako lazima ufikishe dola 10 na google watakutumia (PIN) Kupitia sanduku lako la barua ulilojaza wakati unajiunga nao,

mfano wa PIN utakayotumiwa na google
Ukiingia katika akaunti yako ya adsense kama umeshafikisha dola 10 utaona sehemu wanakuomba ujaze PIN yako waliyokutumia , fanya kama walivyokwambia jaza PIN yako kutoka katika barua hio uliokwenda kupokea posta, ukisha jaza nenda sehemu iliyoandikwa payment setting
Hapo katika setiing kuna vipengele vingi ila sisi tutazungumzia kuhusu kujaza data zako za bank basi, bonyeza new form of payment kisha chagua wire transfer to bank account kisha jaza form utakayopewa ila kabla ya kujaza lazima ujue SWIFF za bank yako kwa hiyo lazima uwasiliane na bank yako ila kama unatumia equity swif zao ni hizi ( $ : EQBLTZTZ, na kwa pesa tofauti na $ ni hii, EQBLKENA)
Picha hii kwa hisani ya ndugu yetu Harsh kumar


baada ya kujaza form yao hiyo baasi utakuwa umeshamaliza kila kitu pindi pesa yako itakapotumwa utajulishwa kupitia email yako na kama unatumia sim banking utajulishwa na sms kutoka bank

Post a Comment

0 Comments