JINSI YA KUJIUNGA NA ADSENSE HATUA KWA HATUA

Habari tena karibu hapa tujuzane haya na yale baada ya kufahamu jinsi ya kujiunga na seebait kama ulipitwa soma hapa Jinsi Ya Kujiunga Na Seebait kutokana na maoni na maombi ya wasomaji wangu nimeona nitimize haja za wasomaji wangu kwa kuwafahamisha kuhusu kujisajili na adsense je unajua adsense ni nini soma hapa jinsi ya kupata pesa kupitia adsense

Tukumbuke kila kitu kina sheria zake na utaratibu wake hivyo ni vema kufamu kuhusu sheria na sera za google , kwanza fahamu ya kuwa adsense hawasapoti lugha ya kiswahili kufahamu zaidi soma hapa sababu za kiswahili kutokubaliwa katika mfumo wa adsense hivyo ikiwa unaweka machapisho kwa lugha ya kiswahili katika blog yako ni vigumu kukubaliwa.

baada ya kufahamu hayo machache nafikiri tuanze lakini unaweza kuniachia maoni yako kama hujaelewa maelezo yangu



Ingia katika blog yako kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa ernings
Utaona sehemu imeandikwa Sign Up for adsense kama huoni na unatumia domain kama SwahiliTech.Net ingia hapa https://www.google.com/adsense/signup watakuletea chagua hili
bonyeza sign in kama umetumia link watakuletea sehemu ya kujaza website yako na lugha lakini kama umetumia blogger moja kwa moja sehemu ya website watakujazia kisha wewe utajaza lugha
lugha zote watakazokuletea hapo zinasapoti mfumo wao kwahiyo ni chaguo lako hapo ila mimi huwa nachagua kiingereza baada ya kuchagua lugha bonyeza Accept association watakuletea muonekano huu
utajaza form hiyo kama wanavyokuomba namba ya simu time zone sehemu ulipo yaani nchi na mkoa jina n.k kisha utasubmit chini kabisa ya hiyo fomu kisha watakuletea muonekano kama huu chini pichani
Bonyeza hapo Continue watakurudisha kwenye dashibodi ya blog yako sehemu ya ernings utaona ujumbe kuwa adsense yako ipo kwenye mchakato itakuwa aproved baada ya muda kidogo, hivyo wataiangalia kama umekidhi vigezo na mashariti yao watakukubalia ndani ya siku tatu na utaona muonekano huu kama utakuwa umekubaliwa
mpaka hapo utakuwa umefanikiwa na kuhusu kupokea pesa zako soma hapa Jinsi ya kupokea pesa yako kutoka adsense mpaka hapo nafikiri utakua umepata muangaza japo kidogo natumaini makala yangu haijakamilika ila wewe unaweza kuikamilisha kwa kuniuliza swali hapo kwenye coment nami nitakujibu ili tukamilishe makala hii, pia sambaza upendo kwa blogger wenzetu kwa kusambaza makala hii nao wajipatie ujuzi huu bure, nimekufahmisha bure basi nawe toa bure

Post a Comment

0 Comments