Hizi Custom domain ni buree yaani haulipii hata senti 10. Utatumia kwa miezi 12 (Mwaka 1) kisha unaiset upya tena. Unaweza kuweka kwenye blog yako hata kama zipo 5.
Makampuni kama Google Adsense na Propeller Ads wanataka blog zenye custom domain kama .com ambayo ni ya kulipia ila kama hauna hela tumia hizi ambazo ni bure Tk, .Ml, .Cf, .Ga, & .Gq
Hatua kwa hatua jinsi ya kupata Free domain na kulink na Blog yako
1. Ingia kwenye website ya
Freenom. Itafunguka kama hapo chini kwenye picha. Sasa Andika jina la blog yako kwenye hicho kibox cheupe. Mfano blog yako inaitwa www.makunyanzi.blogspot.com. Andika Makunyanzi
2. Zitatokea custom za aina mbili yaani za kulipia na za kununua. Chagua za free kwahiyo unaweza chagua .tk, .ml, .cf, .ga, & .gq. Ukishaona unayoitaka bonyeza kwenye kitufe cha Get it now na kisha bonyeza checkout button. Kisha bonyeza Continue
3. Chagua 12 months @ Free. Kisha bonyeza Continue Button
4. Utaletewa form ya Review & Checkout. Andika email yako na kisha bonyeza button ya ku-verify my email Address
5. Ingia kwenye email yako. Na kisha bonyeza link hiyo kama inavyoonekana kwenye picha chini
6. Utaletewa form ya kujaza taarifa zako. Kama inavyooneka kwenye picha hapo chini. Download
Zip Code Pdf kujua Zip code ya mkoa na wilaya. Kisha bonyeza button ya submit ili uweze kutuma taarifa zako
7. Utaletea ujumbe huu kama inavyoonekana hapo chini kwenye picha.
Jinsi ya kulink Free custom domain na blog yako na ionekane www.makunyanzi.tk kutoka www.makunyanzimwilo.blogspot.com.
1. Ingia kwenye blog yako. Kisha scroll down mpaka Settings >> Basic >> Set up a third party URL for your blog. Bonyeza hapo
2. Kwenye kibox cha http// weka jina kama ulivyolisajili kwenye freenom mwanzo (Usibadilishe). Lazima lianze na www.makunyazi.tk kama inavyoonekana kwenye blog. Ukijaribu kusave itakuletea ujumbe "We have not been able to verify your authority to this domain". Usihofu (Usi cancel, acha hivyo hivyo hivyo). Kunywa maji au juice utulize akili maana hapa ndiyo kazi imeanza.
3. Rudi kwenye Website ya Freenom. Bonyeza kwenye Service kisha My Domains. Inaweza kukuomba email na Password. Weka email na Password ili uweze kusign in
4. Bonyeza kwenye Manage Domain
5. Bonyeza Manage Freenom DNS
6. Bonyeza kwenye + More records. Ongeza more record 1 zifike 2.
7. Rudi kwenye blog yako kwenye. Hizi DNS zinatofautiana kwa kila blog kwahiyo usiwe na wasi wasi kwa vile zako hazitofautiani na zingine. 1. Copy www kisha paste kwenye Name, kisha copy ghs.goole.com kisha paste kwenye Target (Chukua ya kwenye blog yako) 2. Copy na ya 2 hivyo hivyo
8. Rudi kwenye Freenom Website
1. Name : www
Type: CNAME (Chagua CNAME ni lazima)
TTL: 14440 (lazima)
Target: ghs.goole.com (Copy kutoka kwenye blog yako kisha i-paste hapo)
2. Copy namba mbili kwenye blog yako kisha ipaste kwenye Name kama inavyooneka. Kwenye TTL weka 14440 na target weka gv-bqgns7kbrh2vf.dv.googlehosted.com Kisha bonyeza Save changes. Itakuandikia Recorded added successfully
9. Add more record tena zifike nne. Kisha jaza taarifa hizo hapo chini. Kisha bonyeza kitufe cha save changes
Type: A
TTL: 300
Target:
216.239.32.21
216.239.34.21
216.239.36.21
216.239.38.21
10. Ukisha bonyeza save changes. Itakuandikia recorded added successfully
11. Rudi kwenye blog yako (Kaa kama dk 5-10). Kisha bonyeza kwenye button ya save. Itakubali. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kulink custom domain na blog yako.
Important Notice
Hizi domain za .tk, .ml, .cf, .ga na gq ni bure kwa miezi 12 (mwaka mmoja) kwahiyo ili uendelee kutumia bure. Ukishajiunga, angalia ni muda gani unakaribia kuisha kwahiyo kabla miezi kuisha yaani umebaki mwezi mmoja, futa domain yako kwenye freenom website kwenye manage Freenom DNS na uanze kuweka domain yako upya. Fuata hatua ya kwanza hadi ya mwisho. Hahitaji kutengeneza account mpya kwahiyo tumia hiyo hiyo.
0 Comments