JINSI YA KUPATA DOMAIN YA .COM BURE KWA MWAKA MMOJA 2022

Leo ntakuonesha namna utakavyoweza kupata domain ya .com bure kwa mwaka mzima na pia hosting ya kudumu bure kabisa ya Tsh. 0.

Fuata hatua zifuatazo kwa usahihi na kwa umakini ili kuvipata hivyo vyote viwili.

1. Fungua akaunti ya Gmail mpya.

* Nenda google andika Gmail Sign up na ukamilishe hili. Sidhani kama hili huwezi eti. Kwahiyo fungua gmail mpya kwanza.

* Utaitumia akaunti hii popote utakapoulizwa email.

2. Nenda tena google andika Yahoo Small Business kisha fungua link ya kwanza kabisa iliyoandikwa Domain Names, Website Builder, Web hosting & More | Yahoo! Small Business , utaona ukurasa kama huu, na kisha bonyeza palipoandikwa LEARN MORE.

3. Utakutana na sehemu imeandikwa START FOR FREE bonyeza hapo na uanze kujaza taarifa zako na za biashara yako.

4. Ukimaliza kujaza taarifa zako, utafika mahali pa kuweka taarifa za malipo, hapa chagua PAYPAL kwa sababu utaweza kuzuia wasikukate hela yoyote pale mwaka 1 utakapopita.

5. Endelea kufuata maelekezo mpaka utafika kwenye ukurasa wa kujaza taarifa za paypal.

  • KUMBUKA: Hawatakukata hata senti 1, kwasababu hii ni programu ya bure kwa kwa mwaka wa 1.
  • PIA: Hakikisha una akaunti ya Paypal iliyothibitishwa la sivyo hutaweza kukamilisha hatua hii kabisa.

6. Ukifanikiwa kukamilisha kuunganisha akaunti yako ya Paypal utaambiwa uhakiki email yako na kwahiyo utafungua inbox utakuta ujumbe wa kuhakiki email fuata maelekezo na ukamilishe hilo.

7. Ukifanikiwa kuhakiki watakuleta kwenye DASHBOARD ya small business, na utaulizwa baadhi ya maswali utahitaji kuyajaza.

  • Sehemu ya namba ya simu, utabuni namba yoyote ya marekani ujaze, maana huwezi kujaza namba ya nchi nyingine yoyote hapo.

8. Ukikamilisha hatua hiyo, nenda semehu ya kuchua domain, pameandikwa “claim and verify domain”.

9. Search domain unayotaka na ubonyeze GET IT NOW , ili kukamilisha usajili wa domain.

10. MUHIMU: Ukikamilisha usajili wa domain, utatumiwa emails kadhaa za kuhakiki domain. Hakikisha unafuata hizo emails na unakamilisha la sivyo domain yako itafungiwa mbeleni.

  • Ujumbe unaweza ukachelewa kidogo kufika ila ukifika hakikisha unakamilisha.

11. Hatua inayofuata ni kuzuia mfumo wao usikate malipo yoyote kwenye Paypal yako mara mwaka mmoja utakapoisha.

  • Utakwenda kwenye paypal yako Kisha fuata maelekezo haya na mtiriko huu:
  • Bonyeza, Sehemu ya Settings > Account Settings > Website Payments > My automatic Payments > Update > My Approoved Payments > Yahoo Aabaco Small Business > Cancel > Yes.

Hii njia ni kwa wale wenye blog za blogspot Kama mimi

Post a Comment

0 Comments