Jinsi ya kutengeneza pesa Mtandaoni


Hapa nitazungumzia kuanzia

1• Freelencing

2• Dropshipping

3• Blogging

4 • Affiliate Marketing

5 • Paid survey

6 • Mwisho tutaangalia websites zinazolipa kwa kuangalia matangazo (Ads).

Sitazungumzia Forex kwasababu imeshajadiliwa hapa sana.

Kwahiyo hizo njia sita (6) ndiyo unatakiwa uzifahamu ili usibabaishwe tena kufahamu njia yakutengeneza pesa online.

Pia niseme wakati naelezea nitajitahidi niguse points zote muhimu kuhusu njia nilizotaja hapo juu ili wewe mwenyewe ufanye maamuzi yako kwakuangalia wapi panakufaa.

Are you ready for this?

Ok, sasa tuanze.

Kwanza kabisa niseme tu sasa hivi kila kitu kinahamia mtandaoni.

Biashara, mashirika, watu binafsi kila mmoja anatafuta namna yakujitengenezea “empire” mtandaoni.

Na hapa lengo ni kutengeneza $$$$ money.

Kama haufahamu namna ya kujiingizia kipato mtandaoni soon you will disappear.

Utashindwa kucompete kwasababu utakuwa nyuma ya teknolojia.

Lakini hili si swala lakuhofia.

Hapa swala lakuhofia ni iwapo utajifunza kutake advantage internet imetoa ama lah.

Sasa baada ya kusema hayo naomba nianze kukupa darasa kwa kila njia niliyotaja hapo juu.

Maelezo haya yatakufanya uwe informed na kamwe hutobabaishwa kufahamu kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani kuhusu kutengeneza pesa mtandaoni.

1 • Freelancing.

Kuhusu Freelancing naomba niwe straight forward kwakusema hii ndiyo njia “sustainable” zaidi kupiga pesa mtandaoni.

Lakini haiishii hapo.

Ukiniuliza freelancers wangapi unaowafahamu wanatengeneza pesa kupitia freelancing nitakujibu nawafahamu wanatengeneza $500 – $1200 a month na pia nawafahamu wanatengeneza $0 a month.

Guess what?

Freelancer wengi hususani from Tz hawana right mindset.

Wengi wanaingia kwenye Freelance platforms with wrong reasons.

Unakuta mtu ameambiwa unaweza tengeneza pesa ndefu kwakuwa transcriber/translator basi huyo mbio anaenda kujiunga with expectations atatengeneza pesa.

No way.

Siku utakapowekeza kwenye skills zako kwanza na kujua mbinu za kuuza ndiyo utakapoweza kutengeneza pesa.

Buyers kwenye Freelance platforms wanafahamu you are not capable to do the work kwa kuangalia tu profile yako.

Na hapa si kwasababu wewe ni biginner, nop. Sababu kuu ni kwamba you are disorganized.

Siyo tu hauwezi kuandaa profile yako vizuri. Pia hujui namna yakuuza ujuzi wako.

You need to learn how to sell.

Period.

JE, NITAFANYAJE KUPATA MTEJA KWA MARA YA KWANZA KAMA FREELANCER?

Ni rahisi but you need to think out side the box.

Kwanza naomba nianze kwa kuuliza swali.

Je, unafikiri ni kitu gani kinamfanya mteja amchague freelancer mwingine na kukuacha wewe?

Jibu ni rahisi.

Good reviews kwenye profile yako.

Freelancer wengi wanaoanza ili kupata trust ya buyers inabidi watafute mtu/watu nakuwaomba kununua service zao na kisha kuwapa review nzuri.

Hapa unatakiwa uwe smart.

Unaweza muomba rafiki au ndugu ajiunge kwenye platform unayotumia halafu anunue huduma yako na kukupa reviews nzuri.

See how it works?

Ukitumia njia ya kawaida kusubiri mteja asiyekufahamu anunue huduma yako wakati huna review hata moja you will likely end up wasting time.

Sikufundishi “umafia”.

Hizi ndiyo mbinu zenyewe za ku-survive as newbie.

Tuendelee…

Je, majukwaa gani ni sahihi kujiunga kama freelancer?

Well, hapa nitapendekeza platforms tatu. Pia kaa mkao wa kula nipo jikoni kuandaa freelance platform ya Kiswahili ambayo itakuwa mahususi kwa wana JF na watanzania. Na mimi binafsi nitakupatia darasa binafsi kukujenga as a freelancer.

Nitumie email through the address kingmediaofficial92@gmail.com

I will respond your mail as fas as possible.

Sasa tungalie majukwaa ya Freelancing.

a • UpWork.com

– hawa wapo vizuri. Job offer ya kwanza kabisa (transcription/translation) nilipatia hapa baada ya kuhangaika katika majukwaa tofauti kwasababu sikuwanafahamu mbinu. Kwenye UpWork nimefanya kazi za watanzania watatu (3). Hehee it was amazing kuona waTz wenzangu nakunipa job offer.

b • Freelance.com

– ninayo account but sijaelekeza nguvu nyingi huko. I have few project I’m working on kwahiyo time yangu inakuwa limited. Ila kwa ufupi ni jukwaa zuri na kongwe. You can try them.

c • Fiverr.com

– nani hapendi Fiverr? Kwenye hili jukwaa unachofanya ni kupost a gig. Gig ni service (huduma) unayouza. Na kila gig inathamani ya $5.

– haiishii hapo. Fiverr wanakuruhusu kupost gigs zenye thamani zaidi kwa mfano $50, $100, $120….ukikidhi vigezo.

Hayo ndiyo majukwaa unavyoweza kujiunga as freelancer.

Unachotakiwa ni kuwa strategic. Fuata tricks nilizokuambia and you will be surprised jinsi ilivyo rahisi.

2 • Dropshipping.

– what should I say about this?

– fuata thread hii mada imezungumziwa kwa kina

3 • Blogging (Kuanzisha blog)

– kamwe usi-underestimate uwezo wa blog kukutengenezea pesa. Binafsi najiona mjinga kwanini sijaanza mapema.

Hebu soma haya maelezo chini ufahamu je kiasi gani unaweza tengeneza.

Haya maelezo ni jibu nililolitoa kwa mwanaJF aliyekuwa anahitaji kuanzisha blog.

“Mkuu kwanza niseme tu kuwa na blog ni njia nzuri yakutengeneza passive income.

Unaweza kutengeneza hadi $500 – $1000 a month.

Kwa kifupi ukiwa na strategy nzuri hiko kiasi ni rahisi kufikia.

Sasa twende taratibu.

Ili blog yako iingize hela kwanza inabidi upate AdSense account toka Google.

AdSense kwa lugha rahisi maana yake umeruhusu google waweke matangazo ya biashara kwenye blog yako.

Na ili google wakupatie AdSense inabidi blog yako iwe imekidhi vigezo.

• haina makala/post zilizo tumika sehemu nyingine.

• umeandika makala zakutosha kwenye blog yako. At least 30 posts.

• makala unazopost kwenye blog yako zina-solve matatizo ya visitors.

Ukiweza kutimiza hivyo vigezo basi unaweza ku-apply for AdSense na ukapata kirahisi.

Naomba niende ndani zaidi.

Baada ya kupata AdSense na matangazo kuonekana kwenye blog yako inabidi uelewe je AdSense itakulipa kiasi gani kwa kila visitor?

Kufahamu hili kwa njia rahisi let’s do the math.

Let’s assume blog yako inapata viewers 1000 kwa siku.

Katika hao viewers 1000 wanao-click matangazo kwenye blog yako ni 200

Pia lets assume kila click inathamani ya $0.10.

Kwahiyo 200 * 0.10

= $20

Hiyo $20 ndiyo unatengeneza kwa hao 1000 viewers.

Kwahiyo kama unauwezo wakupata viewers 30000 kwa mwezi maana yake umetengeneza $600

Lakini kama nilivyosema awali you need guidance”

4 • Affiliate Marketing.

– kwanza kabisa naomba niseme maana ya affiliate Marketing. Hii ni aina ya biashara unayofanya kwa kutafuta wateja na kuwashawishi wanunue bidhaa za kampuni fulani kwa mfano health care products kisha wewe kupata commission.

Kwenye affiliate Marketing utafanikiwa sana iwapo unamiliki blog. Hii inakuwa rahisi kuandika reviews kuhusu product unazopendekeza kwenye blog yako wasomaji watashawishika kununua.

Kingine kuhusu affiliate Marketing nashauri u-promote product zenye commission nzuri. Promote product za makampuni zinazotoa at least 30%.

Kwa mfano ukimshawishi mteja kununua product ya $100 hapo una $30 kama commission.

Kama utashawishi watu 10 tu kwa mwezi basi unaondoka na $300.

Ukibadilisha hii kwa hela yetu ya madafu ni amount nzuri hiyo.

JE, NITAWEZAJE KUWA AFFILIATE MARKETER?

Ni rahisi.

Unachotakiwa kufanya nenda clickbank.

Click bank ni market place ambapo baada ya kujiunga utaweza kuchagua product unayotaka kupromote kama affiliate Marketer.

Kwahiyo kama unataka kuwa affiliate Marketer just go there and create account.

Je, kiasi gani naweza kutengeneza kama affiliate Marketer?

Kujibu swali hili inategemea na idadi ya watu unaoweza kuwafikia na kununua bidhaa kupitia speacial link ambayo ndiyo affiliate link yako.

Kwahiyo hapa unaona iwapo unamiliki blog ni rahisi zaidi kwasababu utaweza kuwashawishi wasomaji.

5 • Paid Survey

– kuhusu Paid Surveys nakushauri uwekeze muda wako kwenye mambo ya maana. Paid Survey wanalipa hela kidogo sana (peanuts). Kwamfano jukwaa kama PaidViewPoint wanalipa $0.03 kwa survey. Kwahiyo unaona kamwe hautoweza kutengeneza chochote.

6 • Website zinazolipa kwa kutazama matangazo (Paid Per Click)

– hii nayo si nzuri sana. Kwamfano NeoBux wanakupa $0.001 kwa kila tangazo utakalo-click. Kwa siku wanaweza kukutumia matangazo hadi 20.

Japo kuna members wanadai wanaweza kutengeneza $30 in a daily basis lakini hii si kwa kitegemea matangazo wanayo-click. Kifupi kuna mbinu hapa na si lengo langu kuelezea leo kwasababu makala itakuwa ndefu sana. Labda naweza kuelezea katika post nyingine.

NENO LA MWISHO.

Nisema tu ili uweze kutengeneza pesa mtandaoni in a constancy manner inabidi ufikirie kujifunza ujuzi unaouzika na ulio kwenye trend.

Jifunze skills hizi na unatengeneza pesa mtandaoni.

1 • SEO

2 • Copy Writing

3 • Content Writing

4 • UX design

5 • Programming

6 • Web development

7 • Transcription & Translation etc.

Kumbuka kujifunza haya yote huitaji muda mrefu. Baadhi ya skills hapo unaweza kujifunza kwa wiki si zaidi ya mbili.

Baada ya kuandika haya yote sasa naomba nimalizie kwakukupata challenge ya kutumiza hayo.

Iwapo unahitaji kujifunza zaidi usisite nitumie email kwenda

kingmediaofficial92@gmail.com

Post a Comment

0 Comments