Naam umekua ukiskia stori za watu mbalimbali,
kuusu biashara hii FOREX.au wewe pia unauzoefu
na biashara hii ya mtandaoni,basi yote kwa yote
leo nakuletea faida na hasara za biashara hii
inayoonekana kukua kwa kasi zaidi,karibu,
FOREX NI NINI??
Ni kifupi cha Foreign Exchange lenye maana
ya ubadilishaji wa sarafu ya nchi moja kuwa
sarafu ya nchi nyingine.mfano ukitoka Tanzania
ukaenda Kenya lazima ubadili pesa zako za
kitanzania kuwa za kenya maana uwezi kutumia Tsh
ukiwa keny.ivyo basi itakubidi ubadilishe
[TSH-KSH]
Kitendo icho cha kubadili pesa za kitanzania
kuwa za kikenya ndio tunaita forex exchange.
Zamani biashara hii ilifanywa na mabenki,
taasisi za kifedha ndani ya serikali za nchi
mbalimbali,,watu matajiri na makampuni
makubwa tu. Lakini kutokana na mapinduzi
ya kiteknolojia.sasa mtu yoyote duniani kote
anaweza kufanya biashara hii mda wowote..
JE HII BIASHARA INA UMUHIMU GANI
KWANGU???
jibu litategemeana na mipango na
malengo uliojiwekea katika maisha yako
lakini unaweza kuifanya
1.kama unataka soko lambalo halilali
2.kama unataka kutengeneza pesa nje ya
kazi au kibarua chako,
3.kama unataka fursa ya kufanya biashara
mda wowote katika siku.
sasa ukiwa na ayo malengo basi FOREX
ni muhimu sana Kwako
NIENDE OFISI GANI AU NI VITU GANI
NAHITAJI NIWE NAVYO ILI NIANZE
KUFANYA BIASHARA YA FOREX???
Kama nilivyokwambia mapinduzi ya technolojia
yametuwezesha mimi na wewe na yule na wale
kufanya biashara hii kwa simu za mikononi tu
{smart phon} au kompyuta ivyo basi ukiwa na
smartphone au kompyuta unaweza kufanya
biashara hii bila buguza yoyote ile wala auhitaji
kwenda ofisi zozote.
FAIDA ZA BIASHARA YA FOREX?
1.UNA UWEZO WA KUFANYA BIASHARA HII
POPOTE ULIPO NA KWA MDA UNAOUTAKA
Uzuru wa biashara hii unaweza kuifanya mda
wowote unaotaka kasoro weekend tu ambapo
soko linafungwa,ivyo basi unaweza kuifanya
kwa urahisi bila kuaribu ratiba zako za kila siku
2.NI BIASHARA AMBAYO HAINA MAKATO
ni moja ya biashara ambayo amna makato ya
kodi kama biashara nyingine zilivyo ivyo basi
ukipata faida yote ni yako aina haja ya makato
ya aina yoyote.
3.SHERIA ZAKE NI RAHISI
yani auhitaji kuwa na degree au masters ili
uweze kuifanya biashara hii,mtu yoyote mwenye
uelewa wa FOREX anaejua kusoma na kuandika
anaweza kufanya biashara hiii
4.UNAWEZA KUYPATA FAIDA KUBWA SANA
NDANI YA MDA MCHACHE SANA
tofauti na biashara nyingine FOREX inaweza
kukupa faida kubwa kwa kuwekeza pesa ndogo
(levarage)
5.UWEPO WA ACCOUNT ZA MAJARIBIO(Demo account)
pia kama umepata uelewa kidogo au unataka uanze
kujifunza biashara hii ni vizuri sana kuwa na Account ya
majaribio ili kuelewa zaidi
Download hapa
izo ndio faida chache kati ya nyingi zilizopo
ndani ya biashara hii.
HASARA ZA BIASHARA YA FOREX.
1.UPATIKANAJI WA HASARA KUBWA NDANI
YA MDA MFUPI
kama zilivyo biashara nyingine pia
forex inafaida na hasara zake ,kwa mda mchache
kuna wimbi la watu wamekua wakiingia katika
biashara hii bila kufanya tafiti kwa kina watu
walioathirika sana ni VIJANA Na hii ni kwasababu
ya kufata mikumbo bila kujua inafanyikaje
hii imepelekea wimbi la watu kuingia hasara
ndani ya mda mchache sanaa
2.INACHUKUA MDA MREFU KUIELEWA VIZURI
Forex ni biashara ambayo ili uielewe vizuri
inaitaji mda wa kutosha na majaribio ya kutosha
tatizo kubwa la vijana ni kutokufanya uchunguzi
wa kina mtu akisimuliwa kidogo anajifanya mjuaji
kesho anaanza ku trade bila elimu ya kutosha hii
imekua ni changamoto kubwa sana katika FOREX
Yote kwa yote kama mtu unania ya kufanya kitu
ni lazima ujitoe kwelikweli hasa ivi vitu vinavyo
weza kukutengenezea pesa,Ivyo basi kama unataka
kuanza biashara hii lazima upate uelewa wakutosha ,
soma vitabu vya kutosha fanya tafiti za kutosha kuusu
biashara hii ukijiona umeijua vizuri ndo uanze kuifanya
vinginevyo utaishia kupata hasara na kuuza vitu vyako
vya muhimu kila kukicha..
usisahau ku
subscribe,like,comment and share
0 Comments