Application 11 Muhimu Za Kutumia Kwenye Simu Yako

Hizi ni Apps 11 muhimu kwa ajili ya simu yako. Kuna apps nyingi za kuweza kutumia ila hizi lazima uwe nazo kwenye simu yako

1. True Caller

Hii app itakayokusaidia kujua majina ya namba mpya inayokupigia (Namba ambazo haujajisave kwenye simu yako)

2. Gesture Lock Screen

Hii itakusaida kujua aliyetaka kufungua pattern au password kwenye simu yako hata ukipoteza simu au kuibiwa. Mwizi akijaribu kufungua password akikosea itampiga picha na kukutumia kwenye email yako.

3. WPS

Hii ni app inafanya kazi kama microsoft office kwenye computer. Utaweza kusoma vitabu zenye format mbali mbali, kuandika na kutengeneza pdf file kwenye simu yako

4. Lucky Patcher

Hii itakusaidia kuondoa matangazo kwenye simu na kui-crack app yoyote ili uweze kutumia bure bila kulipia

5. CamScanner

Hii itakusaidia kupiga picha document zako kama vile vitambulisho, vyeti n.k kuziweka katika mfumo wa pdf au picha. Haina haja ya ku-scann vyeti vyako stationery. Tumia hii app

6. Google drive, Mega au 4shared

Kuna watu wana vitu muhimu sana kama picha, video za matukio mbali mbali, contacts document n.k kwenye simu zao. Kuwa na simu haimanishi vitu vyako vitaendelea kuwepo salama kila siku. Kuna simu kuibiwa au kuharibika. Sasa utafanyaje ili upate vitu vyako hapo ndipo watu huwa wanakumbuka kutafuta data recovery software na hizi haziwezi kurudisha vitu vyako vyote kwa 100%.
Mega, 4shared na Google drive ni online cloud storage ambazo zitakusaidia kuhifadhi vitu vyako online na hata ukipoteza au kuibiwa simu bado utavikuta vikiwa salama. Sign up Google drive, Mega au 4shared uweze kutunza vitu vyako. Wanatoa 15GB bure

7. Blackmart, Aptoide au Ac market

Hii inafanya kazi kama Play store lakini humu utapata apps za bure ambazo play store zinauzwa. Kuna app unaona inauzwa play store $20 lakini hauna pesa na unahitaji sana. Tumia Blackmart, Aptoide au Ac market utaipata

8. Xender

Hii itakusaidia kutuma app, picha na video kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye simu nyingine au kutoka kwenye simu kwenda kwenye computer. Jinsi ya kutuma file zako kwenda kwenye computer

9. Call Recorder

Hii ni app muhimu sana ambayo itakusaida kurecord kila mawasiliano. Kuna wakati unaweza tishiwa maisha na unataka umpeleke mbaya wako polisi kwa sababu amekutukana au kukutishia maisha. Na hauna ushaidi lakini kupitia hii app itarecord kila kitu

10. VLC Media Player

Hii itakusaidia kuplay Video na Audio yenye format yoyote na kuweka subtitle. Kuna wale wapenzi wa movie huwa wanalazimika ku-convert movie ili waweze kuangalia kupitia simu ambapo hupoteza ubora wa movie. Tumia VLC apk haina haja ya kuncovert movie yako

11. YTS

Kuna wakati unapata ugumu wa kudownload movie kupitia simu yako. Download BitTorrent apk au uTorrent apk kisha install kwenye simu yako. Fungua browser yako kisha ingia kwenye website https://yts.su kisha chagua movie unayoitaka. Kisha bonyeza Download button. Ikishamaliza kudownload bonyeza kwenye file ulilolidownload. itakupa option ya kufungulia file lako. Chagua uTorrent apk au BitTorrent apk. Na hapo itaanza kudownload. Jinsi ya kudownload Movie, Series na Animation kwenye simu na computer yakoJinsi ya kuweka subtitle kwenye movie na Series

Post a Comment

0 Comments