Jinsi ya kuroot Simu Yoyote ya Smartphone (Android)


Kuroot simu ni kitendo cha kujipa mamlaka juu ya utumiaji wa simu upendavyo kwahiyo unaweza kubadilisha mfumo wa simu utakao. Unaweza kutoa Application, kubadilisha mwandiko (font) kwenye simu yako.

Muhimu

Kabla ya kuroot simu yako lazima uwe umewezesha Deleoper options na Unkown Source
- Wezesha Developer Options kwenye simu yako kwa kuingia Settings >>> About Phone >>> Build Number. Bonyeza Build Number Mara 7 mpaka ikuletee ujumbe "You are now a Developer". Bonyeza Back Button utaona Developer Option. Ingia hapo kisha weka tiki kwenye USB Debugging Kisha ingia Setting >>> Security >>> Unkown Source. Weka Tiki kwenye Unkown Source.
- Simu yako iwe na chaji 50%

Kuna simu zimefungwa Bootloader na zingine hazijafungwa. Ila simu nyingi hazijafungwa bootloader ni vizuri kabla ya kuroot simu yako uangalie kama imefungwa bootloader. Kuna hizi simu za Huawei Y330 za promotion zimefungwa bootloader.
Bootloader ni mfumo endeshi wa simu ya android na unafungwa ili kumzuia mtu asibadilishe mfumo wa simu kama vile kuinstall custom ROM au kuroot simu.

Kuna simu zenye Secure Boot ambazo huwezi kuroot mpaka uflash kwanza kwa kutumia DA file. Hizi simu zenye mfumo wa Secure Boot humzuia mtumiaji wa simu kubadilisha mfumo wa simu kama kuroot n.k Simu zenye mfumo huu mfano wa simu ya Tecno F1 humzuia mtumiaji kutoingia kwenye File Manager na kuangalia mafaili ya mfumo wa simu kama Bluetooth n.k

Download Secure Boot Download Agent (DA) File
Jinsi ya kuflash Secure Boot Download Agent

Jinsi ya kuroot simu zenye Version ya KitKat (4.4 – 4.4.4) na Lollipop (5.0 – 5.1.1) bila kutumia Computer. (Jinsi ya kuroot simu bila kutumia computer)

1. HTC & INFINIX

Tumia Iroot apk kuroot simu yako

2. SAMSUNG & TECNO, HUAWEI, SONY EXPERIA, LG, VODAFONE,

Kingroot apkPingpong apkKingoroot apkFramaroot apkVroot apk na SRS Root apk,

Jinsi ya kuroot simu kwa kutumia Computer

1. Download Kingoroot exe au Kingroot exe na install kwenye computer (Hakikisha computer yako imeunganishwa na internet). Kisha connect simu yako na Computer kwa kutumia USB Cable. Hakikisha umewezesha Developer Options na Unkown Source kwenye simu yako

Jinsi ya kuroot simu za Samsung

- Download CF AUTO ROOT Files kulingana na model ya simu yako. Kisha Flash kwa Odin
Jinsi ya kuflash CF Auto Root kwenye simu ya Samsung
- Baada ya kuflash. Download Root Checker apk ili kuona kama ipo rooted

Jinsi ya kuroot Vodafone

Jinsi ya kuroot Vodafone VFD 301
Jinsi ya kuroot Vodafone smart tab 3G VFD 1100

SIMU ZENYE ANDROID KUANZIA MARSHALLOW (6.0) MPAKA PIE (9) LAZIMA UFLASH KWA KUTUMIA TWRP KISHA UNAROOT

Google utapata hizi software kulingana na model yako ya simu.

Mahitaji

1. SP Flash tool
2. TWRP recovery imagine 
3. Scatter file for your phone
4. Supersu.zip file

Kisha una root kwa kufuata hatua hizi

A. Copy Superuser.zip kwenye memory card kisha iweke kwenye simu yako
B. Zima simu yako kisha bonyeza Power button+volume up+volume down kwa pamoja ili kuingia kwenye recovery mode
C. Ikishawaka kwenye recovery mode
D. Bonyeza Install, chagua file lako la Superuser.zip uliloliweka kwenye memory card
E. Bonyeza Swipe to flash. Subiri mpaka imalizike kisha itajireboot. Mpka hapo itakuwa tayari
F. Download Supersu apk ili kuhakikisha kama ipo rooted

Post a Comment

0 Comments